Kuhifadhi Nyaraka na kumbukumbu

Taasisi inatoa huduma ya kuhifadhi Hazina na rasilimali za Taifa na  kuhakikisha kwamba rasilimali hizi zinahifadhiwa kwa njia bora na salama, kwa kuzingatia viwango na miongozo ya kimataifa ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.

Kuhaulisha Nyaraka na Kumbukumbu

Taasisi inajukumu la kuhaulisha nyaraka na kumbukumbu kutoka kwenye mfumo wa makaratasi na kuziweka katika mfumo wa kielektroniki. Huduma hii inarahisisha upatikanaji, uhifadhi na usimamizi wa kumbukumbu kwa ufanisi.

Kuhuisha Nyaraka na Kumbukumbu

Taasisi ininajukumu la uhuishaji wa nyaraka ili kuhakikisha zinaendelea kudumu kwa muda mrefu zaidi,pamoja na kunatoa miongozo ya utunzaji na matengenezo ya nyaraka zote zilizoathirika  na ubora kutokana na matumizi ya muda mrefu.

Huduma za Utafiti na ushauri

Taasis inatoa huduma za utafiti na ushauri hutolewa kwa watafiti wenyeji na wageni. Huduma hizo ni pamoja na miongozo na taratibu za kufanya tafiti au taarifa muhimu zinazohitajika. 

Jengo la Ofisi ya Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Kilimani Zanzibar.

IJUE TAASISI YA NYARAKA NA KUMBUKUMBU ZANZIBAR.

Nyaraka na Kumbukumbu ni rasilimali muhimu na ya kipekee (unique and irreplaceable) inayohitaji kutunzwa na kuendelezwa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na baadae. Mbali ya kuwa ni utambulisho wa Taifa, nyaraka na kumbukumbu ni msingi mkuu wa Utawala Bora wa Sheria na Uwajibikaji. Aidha, hazina hii inatoa mchango mkubwa katika kujenga demokrasia,kuondoa rushwa, unyanyasaji, ubadhirifu wa mali, dhulma na vita dhidi ya umasikini.

Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu imeanzishwa na inatekeleza majukumu yake kupitia Sheria ya Kuanzishwa kwa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar Nam. 3, 2008. Jukumu kuu la Taasisi ni kutunza na kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka za Serikali kama Urithi wa Taifa. Pia kusimamia kumbukumbu zote zinazozalishwa na kuhifadhiwa katika taasisi na mashirika ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na taasisi na mashirika ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ofisi zake zilizopo Zanzibar.

Habari na Matukio

MAFUNZO YA UANDAAJI WA DAFTARI LA UHAI WA KUMBUKUMBU

Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar imetoa mafunzo elekezi kuhusu ukusanyaji wa maoni katika uandaaji wa Daftari la Uhai wa Kumbukumbu (Records...

TAASISI YA NYARAKA YAADHIMISHA SIKU YA NYARAKA DUNIANI

Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar leo tarehe 9 Juni 2025 imeadhimisha Siku ya Nyaraka Duniani kwa hafla maalum iliyofanyika katika ukumbi wa...

MAKAMO WA PILI WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO JIPYA LA NYARAKA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imejipanga kufanya mabadiliko na...

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS IKULU AITEMBELEA TAASISI YA NYARAKA

Waziri Ofisi ya Rais – Ikulu, Dk. Saada Mkuya Salum akiambatana na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Ikulu, Ndugu Saleh Juma Musa amefanya ziara katika...

ZIARA YA BODI YA USHAURI TAASISI YA NYARAKA KISIWANI PEMBA

Bodi ya Ushauri wa Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar imefanya ziara ya kikazi  Kisiwani Pemba na kutembelea baadhi za Wizara na Taasisi za umma. Ziara...
Nyaraka ya Juma

Elimika  zaidi kuhusu Nyaraka yetu ya leo...soma zaidi

PUBLIC DOWNLOADS

Muongozo wa Kutathmini na Kuharibu Kumbukumbu

Muongozo wa Usimamizi na Udhibiti wa Kumbukumbu wakati wa Kuzihamisha

Kanuni ya Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu

Sheria Ya Kuanzishwa kwa Taasisi Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar

KUTOKA MAKTABA