Kuhifadhi Nyaraka na kumbukumbu

Taasisi inatoa huduma ya kuhifadhi Hazina na rasilimali za Taifa na  kuhakikisha kwamba rasilimali hizi zinahifadhiwa kwa njia bora na salama, kwa kuzingatia viwango na miongozo ya kimataifa ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.

Kuhaulisha Nyaraka na Kumbukumbu

Taasisi inajukumu la kuhaulisha nyaraka na kumbukumbu kutoka kwenye mfumo wa makaratasi na kuziweka katika mfumo wa kielektroniki. Huduma hii inarahisisha upatikanaji, uhifadhi na usimamizi wa kumbukumbu kwa ufanisi.

Kuhuisha Nyaraka na Kumbukumbu

Taasisi ininajukumu la uhuishaji wa nyaraka ili kuhakikisha zinaendelea kudumu kwa muda mrefu zaidi,pamoja na kunatoa miongozo ya utunzaji na matengenezo ya nyaraka zote zilizoathirika  na ubora kutokana na matumizi ya muda mrefu.

Huduma za Utafiti na ushauri

Taasis inatoa huduma za utafiti na ushauri hutolewa kwa watafiti wenyeji na wageni. Huduma hizo ni pamoja na miongozo na taratibu za kufanya tafiti au taarifa muhimu zinazohitajika. 

Jengo la Ofisi ya Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Kilimani Zanzibar.

IJUE TAASISI YA NYARAKA NA KUMBUKUMBU ZANZIBAR.

Nyaraka na Kumbukumbu ni rasilimali muhimu na ya kipekee (unique and irreplaceable) inayohitaji kutunzwa na kuendelezwa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na baadae. Mbali ya kuwa ni utambulisho wa Taifa, nyaraka na kumbukumbu ni msingi mkuu wa Utawala Bora wa Sheria na Uwajibikaji. Aidha, hazina hii inatoa mchango mkubwa katika kujenga demokrasia,kuondoa rushwa, unyanyasaji, ubadhirifu wa mali, dhulma na vita dhidi ya umasikini.

Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu imeanzishwa na inatekeleza majukumu yake kupitia Sheria ya Kuanzishwa kwa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar Nam. 3, 2008. Jukumu kuu la Taasisi ni kutunza na kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka za Serikali kama Urithi wa Taifa. Pia kusimamia kumbukumbu zote zinazozalishwa na kuhifadhiwa katika taasisi na mashirika ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na taasisi na mashirika ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ofisi zake zilizopo Zanzibar.

Habari na Matukio

Maonesho ya Nyaraka za Kisheria Yaibua Uelewa Mpya kwa Jamii

Katika kuadhimisha Juma la Nyaraka , Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar imeandaa maonesho madogo ya nyaraka za kisheria ikiwa ni sehemu ya...

PBZ Bank Yatwaa Ubingwa wa Nyaraka Day Cup 2026

Mashindano ya Nyaraka Day Cup 2026 yaliyoandaliwa na Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar kama sehemu ya shamrashamra za kuadhimisha Siku ya...

Juma la Nyaraka 2026: Taasisi ya Nyaraka Yawakumbuka Wastaafu na Kufariji Watoto Yatima

Katika muendelezo utekelezaji wa shughuli za jumaa la nyaraka , Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar imefanya ziara maalumu ya kuwatembelea na...

Wadau wakutana katika Jukwaa la Nyaraka 2026 kujadili nafasi ya nyaraka katika kuimarisha uwajibikaji, haki za wananchi na utawala bora.

Katika kuadhimisha Juma la Nyaraka , Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar imeandaa Jukwaa la Nyaraka lililowakutanisha wataalamu mbalimbali...

Mkutano na Waandishi wa Habari

 MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MAADHIMISHO YA JUMA LA NYARAKA ZANZIBAR 2026 Ndugu Viongozi,Ndugu Waandishi wa Habari,Wageni Waalikwa,Mabibi na...

Wanafunzi wa Cohort ya Sita Skuli ya Sheria Zanzibar Wafanya Ziara ya Kimasomo Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar

Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar imepokea ugeni wa wanafunzi wa Cohort ya sita mwaka wa masomo 2026/2027 kutoka Skuli ya Sheria Zanzibar (The...
Nyaraka ya Juma

Elimika  zaidi kuhusu Nyaraka yetu ya leo...soma zaidi

PUBLIC DOWNLOADS

Muongozo wa Kutathmini na Kuharibu Kumbukumbu

Muongozo wa Usimamizi na Udhibiti wa Kumbukumbu wakati wa Kuzihamisha

Kanuni ya Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu

Sheria Ya Kuanzishwa kwa Taasisi Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar

KUTOKA MAKTABA